| ← 1Timothy (5/6) → |
| 1. | Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu; |
| 2. | wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote. |
| 3. | Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli. |
| 4. | Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu. |
| 5. | Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku. |
| 6. | Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai. |
| 7. | Mambo hayo pia uyaagize, ili wasiwe na lawama. |
| 8. | Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini. |
| 9. | Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja; |
| 10. | naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema. |
| 11. | Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa; |
| 12. | nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza. |
| 13. | Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa. |
| 14. | Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu. |
| 15. | Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. |
| 16. | Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli. |
| 17. | Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. |
| 18. | Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake. |
| 19. | Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. |
| 20. | Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. |
| 21. | Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo. |
| 22. | Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi. |
| 23. | Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara. |
| 24. | Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata. |
| 25. | Vivyo hivyo matendo yaliyo mazuri ya dhahiri; wala yale yasiyo dhahiri hayawezi kusitirika. |
| ← 1Timothy (5/6) → |