← 1Timothy (2/6) → |
1. | Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; |
2. | kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. |
3. | Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; |
4. | ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. |
5. | Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; |
6. | ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. |
7. | Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli. |
8. | Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. |
9. | Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; |
10. | bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. |
11. | Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. |
12. | Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. |
13. | Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. |
14. | Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. |
15. | Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi. |
← 1Timothy (2/6) → |