| ← 1Corinthians (10/16) → |
| 1. | Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; |
| 2. | wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; |
| 3. | wote wakala chakula kile kile cha roho; |
| 4. | wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. |
| 5. | Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. |
| 6. | Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. |
| 7. | Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. |
| 8. | Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. |
| 9. | Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. |
| 10. | Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu. |
| 11. | Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. |
| 12. | Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. |
| 13. | Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. |
| 14. | Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. |
| 15. | Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. |
| 16. | Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? |
| 17. | Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. |
| 18. | Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? |
| 19. | Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? |
| 20. | Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. |
| 21. | Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. |
| 22. | Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye? |
| 23. | Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo. |
| 24. | Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake. |
| 25. | Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; |
| 26. | maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo. |
| 27. | Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri. |
| 28. | Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri. |
| 29. | Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? |
| 30. | Ikiwa mimi natumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho? |
| 31. | Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. |
| 32. | Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu, |
| 33. | vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa. |
| ← 1Corinthians (10/16) → |