| 1Chronicles (1/29) → |
| 1. | Adamu, na Sethi, na Enoshi; |
| 2. | na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; |
| 3. | na Henoko, na Methusela, na Lameki; |
| 4. | na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi. |
| 5. | Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. |
| 6. | Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. |
| 7. | Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani. |
| 8. | Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. |
| 9. | Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. |
| 10. | Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. |
| 11. | Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, |
| 12. | na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. |
| 13. | Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; |
| 14. | na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; |
| 15. | na Mhivi, na Mwarki, na Msini; |
| 16. | na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. |
| 17. | Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. |
| 18. | Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. |
| 19. | Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. |
| 20. | Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; |
| 21. | na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; |
| 22. | na Obali, na Abimaeli, na Sheba; |
| 23. | na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. |
| 24. | Shemu, na Arfaksadi, na Sala; |
| 25. | na Eberi, na Pelegi, na Reu; |
| 26. | na Serugi, na Nahori, na Tera; |
| 27. | na Abramu, naye ndiye Ibrahimu. |
| 28. | Wana wa Ibrahimu; Isaka, na Ishmaeli. |
| 29. | Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; |
| 30. | na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; |
| 31. | na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. |
| 32. | Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani. |
| 33. | Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura. |
| 34. | Na Ibrahimu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli. |
| 35. | Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. |
| 36. | Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. |
| 37. | Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. |
| 38. | Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. |
| 39. | Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani. |
| 40. | Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. |
| 41. | Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. |
| 42. | Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani. |
| 43. | Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. |
| 44. | Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake. |
| 45. | Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake. |
| 46. | Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. |
| 47. | Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake. |
| 48. | Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake. |
| 49. | Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake. |
| 50. | Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akamiliki badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. |
| 51. | Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; |
| 52. | na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; |
| 53. | na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; |
| 54. | na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu. |
| 1Chronicles (1/29) → |